Jamii FM

 Wazazi  kikwazo  watoto  kumaliza elimu ya msingi Mtwara DC

16 April 2024, 08:55 am

Wazazi na Wananchi kutoka viijiji vya kata ya mkunwa wakijadili changamoto za Elimu kwa watoto wao(Picha na Musa)

Wazazi wengi wamekuwa wakiweka nguvu kubwa kwenye mila ya Jando na unyango kuliko Elimu

Na Musa Mtepa

Inaelezwa kuwa Wazazi kutotambua umuhimu wa Elimu ndio chanzo cha Watoto  wengi kutomaliza Elimu ya Msingi katika Halmashauri ya Mtwara Vijijini.

Wakizungumza na Jamii Fm Radio Wananchi wa kata ya Mkunwa Halmashauri ya Mtwara vijijini mkoani Mtwara  wamesema kuwa Wazazi wengi wamekuwa wakiweka nguvu kubwa kwenye mila ya Jando na unyango kuliko Elimu.

Bi Stella Kasiani Mzazi na mkazi wa Kijiji cha Mkunwa amesema kumekuwa na tabia ya Wazazi kuwapeleka Watoto Jandoni kipindi ambacho  bado masomo yakiwa yanaendelea huku akiiomba Serikali kuweka sheria na kuwachukulia hatua kwa Wazazi wenye tabia kama hiyo.

Sauti ya Bi Stella Kasiani Mkazi wa Kijiji cha Mkunwa Mtwara Vijijini

Aidha Kwa upande wa Bakari Hamisi mkazi wa kjiji cha Miwindi ameziomba serikali za Vijiji Kusimamia na kuthibiti ufanyikaji holela wa Mila za jando za unyago ili kuwaokoa Watoto wanaokosa Masomo wakiwa kwenye sherehe hizo.

Sauti ya Bakari Hamisi mkazi wa Kijiji cha Miwindi Mtwara vijijini

Kwa upande wake Afisa Mtendaji  wa kata ya Mkunwa Aroun Parselaw amesema kuwa ili kukabiriana na chanagamoto hiyo wao kama serikali ya kata watapanga ratiba na utaratibu rafiki juu ya sherehe  za jando na unyago kufanyika kwa tarehe maalumu itakayopangwa.

Sauti ya Aroun Parselaw afisa mtendaji kata ya Mkunwa