Jamii FM

Bodi ya wakurugenzi TANESCO yafanya zira Mtwara

5 May 2021, 12:33 pm

Na Gregory Millanzi

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Dkt Alexander Kyaruzi akiambatana na wajumbe wa bodi hiyo, amewataka wawekezaji kuwekeza Mtwara na Lindi kutokana na uwepo wa Nishati ya umeme wa kutosha.

Amesema kuwa serikali ilinunua mashine mbili za kufua umeme zenye uwezo wa kuzalisha megawati 4.3 kila moja na kufanya kituo cha Mtwara kiongeze uzalishaji mpaka kufikia megawati 8.6 baada ya mitambo hiyo kuwepo mkoani hapa.

Wajumbe wa Bodi katika ziara

Dkt Kyaruzi na wajumbe wa bodi wametembelea kijiji cha Kisiwa kilichopo kata ya Naumbu halmashauri ya wilaya ya Mtwara ambapo Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) itajenga mitambo ya uzalishaji yenye uwezo wa megawati 300.

Mitambo iliyotembelewa na wajumbe wa bodi

Kwa sasa kituo cha uzalishaji umeme Mkoani Mtwara kina mitambo 11 kati ya 13 inayofanya kazi, na kwa sasa kituo kinazalisha megawati 26 na mahitaji ya mkoa wa Mtwara na Lindi ni megawati 18.

Dkt Kyaruzi amefurahishwa na utendaji kazi wa Tanesco mkoa wa Mtwara na kuwaagiza wahakikishe wanaimarisha utendaji kazi ili kuwafikishia wananchi nishati ya umeme.Kamati ya bodi ya wakurugenzi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO) inafanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara kwa kutembelea miradi ya umeme na wanaendelea na ziara katika mikoa ya Ruvuma na Lindi.