Jamii FM

Door of hope yatoa msaada kwa ajili ya siku ya Wanawake Duniani

6 March 2021, 14:15 pm

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Leo 6, Machi 202, taasisi ya Door of Hope Tanzania imekabidhi kilo 200 za Mchele kwenye Halmashauri ya Mtwara Mikindani chini ya Idara ya Maendeleo ya jamii kama sehemu ya kuwashika mkono wanawake waliopata athari za mafuriko.

Pichani ni Mkurugenzi wa Door of Hope Tanzania na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na Maafisa

Kila ifikapo tarehe 8 Machi kila mwaka huadhimishwa siku ya wanawake Duniani siku ambayo huadhimishwa kwa matukio mbalimbali.

M

koa wa Mtwara utaadhimishwa kwa matukio tofauti likiwemo la chama cha waandishi wa Habari mkoani hapa (MTPC) watapeleka msaada wa taulo za kike katika shule ya sekondari ya wasichana ya masista Manispaa ya Mtwara Mikindani.