Jamii FM

Mwenyekiti CCM Mtwara Vijijini awataka wenyeviti wa vijiji kuwatumikia Wananchi

12 December 2024, 13:44

Mwenyekiti wa CCM Mtwara vijijini Nashir Pontiya akizungumza na Wanachama na Wananchi wa kijiji cha Nyengedi kwenye hafla ya kushukuru na kumpongeza Bi Lukia Mnyachi Mwenyekiti pekee wa kijiji wa kike katika kata ya Mkunwa (Picha na Musa Mtepa)

Hii ilikuwa sherehe za kumpongeza Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi Bi Lukia Mnyachi baada ya kuchaguliwa na Wananchi katika nafasi hiyo.

Na Tatu  Mshamu

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mtwara Vijijini, Nashiri Pontiya,amewataka wenyeviti wa vijiji waliochaguliwa kupitia chama hicho kuacha kukidharau chama hicho baada ya kuchaguliwa huku akisisitiza umuhimu wa viongozi hao kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kutumia kamati za maendeleo ili kuhakikisha manufaa kwa wananchi waliowachagua.

Ameyasema hayo December 11,2024 akiwa mgeni rasmi  katika hafla  iliyoandaliwa na wanachama wa CCM Kijiji cha Nyengedi kufurahia ushindi wa viongozi hao, na kuwasilisha  changamoto zinazowakabili katika Kijiji  hiyo, ikiwa  ni ukosefu wa maji,shule,zahanati pamoja na soko.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara Vijijini.

Katika hafla hiyo, Bi.Lukia Mnyachi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi, ametoa shukrani kwa wananchi kwa kumuamini na kumchagua, huku akiahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo bila kujali itikadi za vyama.

Sauti ya Lukia Mnyachi Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi

Mwenyekiti wa UWT (CCM) Wilaya ya Mtwara, Bi. Mwajuma Nahembe, amewakumbusha wazazi kusimamia malezi ya watoto wa kike ili kuwaepusha na vitendo hatarishi wakati wa likizo, ili wasikose masomo.

Sauti ya 1 Mwajuma Nahembe mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mtwara.
Mwajuma Nahembe mwenyekiti wa UWT (CCM) wilaya ya Mtwara(picha na Musa Mtepa)

Zuhura Farid, Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Mtwara, amesisitiza umoja kati ya viongozi waliochaguliwa katika Kata ya Mkunwa na kuwataka kuondoa makundi yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi, ili kuwatumikia wananchi kwa umoja.

Sauti ya 2 Zuhura Farid Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Mtwara
Zuhura Farid Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Mtwara akizungumza kwenye hafla ya kumpongeza mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi (Picha na Musa Mtepa)