Jamii FM

Mvua yasababisha mafuriko Mtwara Mjini

12 January 2021, 12:46 pm

Kufuatia mvua zilizoanza kunyesha alfajiri ya leo January 12, 2020 mkoani Mtwara, barabara katika maeneo mengi ya Manispaa ya Mtwara Mikindani zimefurika pia  nyumba kuingiwa na maji.

Baadhi ya maeneo yaliyoatiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ni pamoja na Kituo kikuu cha Mabasi Chipuputa, Soko la chuno, Kiyangu, kiyanga, chuno, na katika baadhi ya maeneo ya kata ya Naliendele.

Aidha,Mali za baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo pia zimeathirika.

Siku ya January 09,2021 Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania  ilitoa taarifa ya uwepo wa mvua ukubwa  na Upepo mkali.