Jamii FM

Timu ya Mtoto Kwanza yatambulishwa Mtwara

13 July 2023, 15:35 pm

Na Gregory Millanzi

“Sisi kwenye mkoa wetu huu watoto wana shida kubwa ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia, najua kupitia KIMAS na mradi huu utapambana na hatari zote ambazo zinatokana na hawa watoto, pia itaongeza uelewa wa malezi na makuzi ya awali ya mtoto hasa tukianzia akiwa tumboni”

Timu ya Mtoto Kwanza wanaotekeleza programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) 2021/2022- 2025/2026 kwa mkoa wa Mtwara wamefika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara kujitambulisha.

Katibu tawala mkoa wa Mtwara Abdallah Malela akikabidhiwa kitabu cha programu ya PJT-MMMAM na meneja wa taasisi isyokuwa ya kiserikali ya Kitovu cha Maendeleo Safi (KIMAS) Torai Kibiti, baada ya kufika ofisi ya mkoa kujitambulisha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo. (Picha na Gregory Millanzi)

Shirika lisilo la kiserikali la Kitovu cha Maendeleo Safi (KIMAS) ya mkoani hapa, Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mtwara, na Mwandishi kinara wa masuala ya watoto wamejitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Abdallah Malela.

Katibu tawala wa Mkoa wa Mtwara Abdallah Malela amesema program hii ikitelezwa vizuri, itasaidia sana mkoa wa Mtwara hasa kwenye malezi na makuzi ya awali ya mtoto.

Sauti ya Abdallah Malela Katibu tawala Mkoa wa Mtwara

Na kwa upande wake Meneja wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Kitovu cha Maendeleo safi (KIMAS) Torai Kibiti amesema ameshukuru kwa ukaribisho wa ngazi ya mkoa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mtoto kwanza na kwakushirikiana na wadau wengine watahakikisha wanafanikisha mradi wa mtoto kwanza unafanya vizuri na kuongeza uelewa wa jamii kwenye Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Programu hii ina malengo makuu manne mojawapo ni kuwajengea uwezo walezi, Familia na jamii ili watekeleze taratibu bora za malezi jumuishi kwa watoto wenye umri wa miaka 0 mpaka 8