Jamii FM

TFS yaombwa kutoa elimu ya huduma za misitu

29 March 2024, 17:46 pm

Mwenyekiti wa kijiji cha Namahyakata Shuleni akiwa na mahojiano na Mwandishi wa jamii fm Radio(Picha na Musa Mtepa)

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wameombwa  kutembelea vijiji na kutoa Elimu kwa Wananchi  ili wapate uelewa juu ya athari zinazo weza kujitokeza kutokana na  matumizi mabaya  ya Mazao ya Misitu

Na  Musa  Mtepa

Akizungumza na Jamii Fm Radio 28/3/2024 Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi Halmashauri ya Mtwara vijijini  Bw Salumu Mtunuma amesema kuwa ili wananchi wapate uelewa juu ya athari hasi za matumizi mabaya ya misitu TFS wanatakiwa kwenda vijijini na kutoa elimu kwa Wananchi  na sio kusimama kwenye Vizuizi vya Barabarani na Mitaani  kukamata  wauazaji wa mkaa.

Sauti ya 1  Bw Salumu Mtunuma  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi

Aidha Bw Mtunuma amesema kuwa hali ya Mazingira vijijini sio mzuri kutokana na Watu kuingia kwenye Biashara  ya mkaa  kunakosababisha kupoteza miti  na misitu mikubwa pamoja na kupoteza vyanzo vya  Asili vya maji .

Sauti ya 2  Bw Salumu Mtunuma  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi

Naye Mwenyekiti wa kijiji  cha Namahyata Shuleni  Azizi Mbotani amesema  kukusanya Wananchi wengi kwa wakati mmoja kunaweza kuwa na gharama kubwa hivyo serikali na TFS wanaweza kutoa Elimu kwa  Wenyeviti na Watendaji wa vijiji ili wao waweze kuwaelimisha Wananchi katika mikutano yao.

Sauti ya Azizi Mbotani Mwenyekiti wa kijiji cha Namahyakata Shuleni

Kwa upande wake Peter Christopha  Nguyenje  Muhifadhi Mwandamizi kutoka ofisi ya wakala wa huduma ya misitu (TFS) Wilaya ya Mtwara  amesema kuwa misitu ni mali ya watu  wote hivyo ni jukumu la kila mmoja kutunza na kusimamia ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoweza kujitokeza.

Sauti ya Peter Christopha  Nguyenje  Muhifadhi Mwandamizi kutoka ofisi ya wakala wa huduma ya misitu (TFS) Wilaya ya Mtwara.