Jamii FM

Viongozi wa Dini wasisititwa kupiga vita tabia chafu

22 March 2023, 12:38 pm

Viongozi wa dini katika kikao cha Dua maalum. Picha na Musa Mtepa

Watanzania hawana tabia ya ndoa za jinsia  moja hivyo tamaduni za nje zisiruhusiwe kuingia nchini  huku akiwataka jamii kupiga vita madangulo yote yanayofanya biashara ya ngono

Na Musa Mtepa

Jamii na Viongozi wa Dini wametakiwa kuwa mstari wa mbele  kupiga vita tabia chafu ambayo haipo katika mila na Desturi  ya kitanzania .

Akizungumza na Mashekhe waliojitokeza  kwenye Dua ya kumuombea Rais wa jamhuri ya muungano wa Dr Samia Suluhu Hassani  kutimiza miaka miwili madarakani  viwanja vya mashujaa Manispaa ya Mtwara Mikindani, mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi  mkoa wa Mtwara  Saidi Musa Nyengedi amesema kuwa Watanzania hawana tabia ya ndoa za jinsia  moja hivyo tamaduni za nje zisiruhusiwe kuingia nchini  huku akiwataka jamii kupiga vita madangulo yote yanayofanya biashara ya ngono.

Aidha Mwenyekiti amesema kuwa mmomonyoko wa maadili  ni mkubwa hivi sasa  mataifa ya nje yanataka  kuharibu mila na Desturi za kiafrika hivyo viongozi wa Dini ,Wazee akina Baba na  mama wawe mstari wa mbele kupiga vita tabia hizo chafu.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Saidi Musa Nyengedi

Kwa upande wa viongozi wa Dini Mkoani Mtwara wameitaka jamii wasiwe tayari kukubali kuingiliwa na mambo yasiyostahili  katika mila na desturi za nchi huku wakipinga kuwa hakuna Dini inayotoa haki kwa mapenzi ya jinsia moja.

Sauti ya viongozi wa Dini, Shekhe wa wilaya Mtwara MC Abdallah Ally Hemed