Jamii FM

Manispaa ya Mtwara Mkindani yapitisha Rasimu ya Bajeti ya TARURA zaidi ya shilingi Bilioni 5

11 January 2022, 16:49 pm

Hali ya Barabara  zinazosimaniwa na TARURA ni ya kuridhisha, japo mtandao wa barabara kwa asilimia kubwa ni barabara za udongo ambazo huathiriwa  kwa kiasi kikubwa kipindi cha mvua.

Mhandisi Hatibu Nunu

Baadhi ya Madiwani wakiwa katika moja ya vikao vya kiutendaji; Picha kutoka maktaba ya Jamii fm

Na Gregory Millanzi

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara, limepitisha Rasimu ya Bajeti ya Matengenezo ya barabara kupita kwa Wakala wa Barabara za vijijini na Mijini (TARURA) kwa zaidi ya shilingi Bilioni 5 (5,031,300,000.00)kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti ya Matengenezo ya  Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mtwara  Mhandisi Hatibu Nunu amesema, Wanasimamia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilomita 1,522.64 kati ya hizo 60.27 ni za lami, Kilomita 367.14 ni za Changarawe na Kilomita 1,095.23 ni za udongo na jumla ya vivuko mchanganyiko ni 1247 .

Mhandisi Nunu amesema kuwa, Hali ya Barabara  zinazosimaniwa na TARURA ni ya kuridhisha, japo mtandao wa barabara kwa asilimia kubwa ni barabara za udongo ambazo huathiriwa  kwa kiasi kikubwa kipindi cha mvua.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Mtwara Mhandisi  Hatibu Nunu amesema, watahakikisha kuwa Barabara zinapitika kwa kutumia Rasilimali zilizopo, pia ameongeza kuwa kupitika kwa barabara kunategemea itaendelea kuimarika kwa kadri matengenezo ya barabara yatakavyokuwa yanaimarishwa kila Mwaka.

Tutahakikisha kuwa Barabara zinapitika kwa kutumia Rasilimali zilizopo, pia kupitika kwa barabara kunategemea kuendelea kuimarika kwa kadri matengenezo ya barabara yatakavyokuwa yanaimarishwa kila Mwaka.

Mhandisi  Hatibu Nunu

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani  Shadida Ndile aimeipongeza TARURA kwakugusa kila eneo kutokana na bajeti ilivyo nah ii inaleta picha kuwa kwa upande wa Manispaa itasaidia kumaliza changamoto za Barabara.

Mstahiki Meya  Ndile amewashauri TARURA kuhakikisha kuwa Ujenzi na ukarabati wa Barabara unaenda sawa na ujenzi wa Mitaro ya kupitishia maji Barabarani ili kuhakikisha barabara zinadumu kwa muda mrefu kwani barabara nyingi zinaharibika wakati wa msimu wa Mvua.