Jamii FM

Anayefahamu Tiba Asilia ya Magonjwa Upumuaji afike ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.

22 February 2021, 12:50 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametoa wito kwa wananchi mkoani hapa kwa Anayefahamu tiba asilia ya magonjwa ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya pumu na magonjwa ya mfumo wa hewa na mwenye dawa asilia zenye kutibu magonjwa hayo, wajitokeze ofisini kwake ili waweze kupewa utaratibu wa namna ya kuwatibu wanaohitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 22 Februari 2021 na kuwaasa wananchi kuhakikisha wanajitokeza ili kuhakikisha kile wanachokifanya kipewe kipaumbele hasa kwenye tiba asilia na kuweza kuitangaza ili kuwasaidia wenye matatizo ya magonjwa ya upumuaji.

Pia ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya kushona barakoa kwa ajili ya kuwauzia wale wanaotumia kwa ajili ya kujikinga na kuchukua tahadhari ya Corona.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amewataka wananchi kuwa na mazoea yakufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa Corona.