Jamii FM

SDA yapaza sauti juu ya unyanyasaji wa kijinsia

17 February 2022, 23:46 pm

Na Amua Rushita

Shirika la maendeleo ya michezo (SDA) Mtwara kupitia mradi  wa  kuwawezesha wabinti kupaza sauti, wameendesha Semina ya siku mbili juu ya kuwapa elimu ya namna ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, semina hiyo imefanyika katika  ukumbi wa chuo cha Montesory  leo  februari 16 -17, 2022.

mmoja wa wawezeshaji wakiendelea na semina

Akizungumza na Jamii fm, Mratibu wa mradi huo Bi. Jackline mpunjo amesema semina kama hiyo inafanyika katika kila halmashauri iliyopo mkoani mtwara ili kuwajengea uwezo mabinti, waalimu na makungwi katika kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani, wameamua kuwapa elimu hiyo ili waweze kupunguza mimba za utotoni na kuongeza ufaulu wa masomo shuleni, Pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kugawa taulo za kike zaidi ya 450  kwa shule hamsini (50) wanazofanya nazo kazi, na taulo hizo ni rafiki kwa  mazingira ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

ripoti maalumu juu ya semina elekezi kuhusu unyanyasaji wa kijinsia

Shirika hilo la Maendeleo ya  Michezo (SDA) inashirikiana na serikali bega kwa bega ili kuhakikisha wanafikia malengo kwa kushirikiana na halmashuri zote za mkoa wa mtwara pamoja na dawati la jinsia.