Jamii FM

Watumishi wa umma watakiwa kufanya kazi kwa weledi

22 April 2024, 16:30 pm

Baadhi ya watumishi wa umma wakifuatilia kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Benki kuu BOT Mtwara(Picha na Mwanahamisi Chikambu)

Inaonesha kumekuwa na ongezeko la vitendo vya utovu wa nidha kwa  watu wa umma wakiwa kazini ikiwemo Rushwa na upungufu wa maadili.

Na Mwanahamisi Chikambu

Kamishina wa utumishi umma  Balozi John Haule amewataka watumishi wa umma mkoa wa Mtwara

kufanya kazi kwa waledi na kuwataka  kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi

wa umma.

 Balozi John Haule ameyasema hayo leo  tarehe 22-04-2024 katika ufunguzi wa kikao

kazi kati ya tume na mamlaka za serikali za mitaa Kilichowakutanisha watumishi wa umma kutoka katika

taasisi mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania BOT tawi la Mtwara lengo ni kuwajengea uwezo watumishi wa serikali katika kuzitafsiri, kuzielewa sheria na taratibu zinazosimamia utumishi wa umma .

Aidha Balozi John Haule amesema kuwa riporti ya robo mwaka zinazowasilishwa kutoka kwa waajiri

inaonyesha kuwa idadi ya watumishi wa umma wanaochukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukiuka

maadili ya utumishi imeongezeka.

Sauti ya 1 Balozi John Haule Kamishina wa utumishi wa umma

Pia amewaomba watumishi wa umma kujiepusha na vitendo  vya utovu wa nidhamu, kama vile

uombaji wa rushwa, uzembe, na utoro kazini ili wananchi wapate huduma zinazostahili.

Sauti ya 2 Balozi John Haule Kamishina wa utumishi wa umma
Baadhi ya watumishi wa umma mkoani Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja na kamishina wa utumishi wa umma Balozi John Haule Katika ukumbi wa BOT Mjini Mtwara.(Picha na Mwanahamisi Chikambu)

Mada zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho ni majukumu ya mamlaka ya tume ya utumishi wa umma,

haki na wajibu wa mtumishi na mwajiri, maadili katika utumishi wa umma, huku kauli mbiu ikisema kuwa

uzingatiaji wa sheria,haki na wajibu kwa kila mtumishi mwajiri na mamlaka nidhamu ndio msingi wa

ufanisi wa utumishi wa umma.