Jamii FM

Makala: Fahamu namna dawa za kulevya zinavyomuathiri mtoto tumboni

8 April 2023, 13:28 pm

Wataalamu wakitoa elimu juu ya athari za dawa za kulevya. Picha na Gregory Millanzi.

Mama mjamzito akiwa anatumia madawa ya kulevya zinamuathili mama mwenyewe na kwenye mfumo wake wa  uzazi na kupelekea mtoto kuathirika moja kwa moja kama ambavyo mama anaathirika kwa dawa hizo, na kupelekea mtoto kuwa na uraibu na wakati mwingine husababisha vifo kwa mama mjamzito wakati wa kujifungua.

Maisha ya mtoto huanzia tumboni na Mama mjamzito hutakiwa kulinda mtoto tangu akiwa tumboni, katika makala haya tunaangazia madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya kwa mama mjamzito na sheria ya adhabu kwa mtu atakayekutwa nayo.

Sikiliza makala haya ili kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu athari za mzazi anayetumia dawa za kulevya.

Sikiliza makala haya yaliyoandaliwa na Gregory Millanzi na kusimuliwa na Mwanahamisi Chikambu.