Wazazi kwenye wiki ya elimu
Jamii FM

Waandika barua ya kuacha shule kisa kiingereza

4 March 2023, 14:39 pm

Ofisa Elimu Ndg. Benjamini Ndosi. Picha na Musa Mtepa

Na Musa Mtepa

Wanafunzi wa kidato cha Kwanza kwa mwaka 2023 na vidato vya juu katika kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani wamekua wakijitokeza na wazazi wao ofisi ya mkuu wa shule ya Sekondari Naliendele wakiwa na Barua ya kuacha shule kwa sababu ya kutoelewa kiingereza.

Akizungumza hayo na Jamii fm Radio ofisa Elimu Ndg. Benjamini Ndosi katika Wiki ya Elimu amesema pia hitaji la wanafunzi hao ni kwenda kupata Elimu ya ufundi.

“Nina wasi wasi kuwa huenda huko nyumbani wanakuwa tayari wameshakubaliana mtoto na mzazi kuandika Barua ya kuacha shule kwa kisingizio cha elimu ya ufundi.”

Sambamba na hilo Ndg. Ndosi amesema kuwa sababu kubwa inayosababisha kuwepo kwa tabia hiyo ni kutokuwa na utayari wa kusoma na kufuata makundi rika huku akisistiza manispaa imekuwa ikiweka mazingira wezeshi ya kumfanya mwanafunzi anaelewa kinachofundishwa kwa kuwapatia elimu ya utangulizi dhamira ikiwa kuwawezesha kukifahamu kiingereza.

Nina wasi wasi kuwa huenda huko nyumbani wanakuwa tayari wameshakubaliana mtoto na mzazi kuandika Barua ya kuacha shule kwa kisingizio cha elimu ya ufundi.

Aidha amewataka wazazi wa Naliendele kushirikiana katika kuwajibika ili kuleta maendeleo katika elimu kwa kuchangia chakula kwa ajili ya Wanafunzi ,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa watoto wao na kushirikiana katika kudhibiti utoro.

Lakini pia kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa kufika hadi shuleni na ikiwezzekana hata kumuuliza mwalimu juu maendeleo ya mtoto husika na kupata ushuri.