Jamii FM

DC Kyobya: tudumishe Amani

8 May 2021, 06:47 am

Na Karim Faida

Mkuuu wa wilaya ya Mtwara Ndugu Dunstan Kyobya amewataka wananchi kuendelea kulinda amani ya Mtwara na kutoa taarifa kwa mamlaka pindi wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

DC Kyobya akizungumza wakati wa hafla hiyo

Ndugu Kyobya amesema hayo jana Mei 7 2021 katika hafla fupi baada ya kuandaa Futari kwa viongozi wa Dini, viongozi wa kisiasa, viongozi wa serikali, waandishi wa habari na wageni wengine akishirikiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara mikindani Bi Shadida Ndile iliyofanyika nyumbani kwa mkuu huyo wa wilaya ambapo amesisitiza ushirikiano uendelee kwa ajili ya kuijenga Mtwara.

Kwa upande wake Shekh Saidi Mkopi aliyekuja kumuwakilisha Shekh mkuu wa mkoa wa Mtwara Shekh Nurdin Mangochi, amesema kitendo alichokifanya mkuu wa wilaya ni cha kuigwa na ni faida kubwa kwake pia inasaidia kuongeza upendo kati yetu.

Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria

Nae Hasnein Murji, mfanyabiashara wa mkoa wa Mtwara aliyekuja kuwawakilisha wafanyabiashara amesema kitendo cha mkuu wa wilaya na Meya kuwakutanisha katika ftari hiyo inaonesha utayari wa viongozi hao hata katika kuwepokea na kuwapa ushirikiano wawekezaji waliopo Mtwara na watakaokuja kwa ajili ya kuwekeza kibiashara.

Akiongea na Jamii fm Radio baada ya kumalizika kwa Hafla hiyo Mstahiki meya Bi Shadida Ndile ambae ameshirikiana na mkuu wa wilaya kuandaa ftari hiyo, amesema amefurahishwa kwa mahudhulio mazuri na kuomba mshikamano uendelee kwa maslahi mapana ya Mtwara.