Jamii FM

TPA yaiomba serikali Bandari ya Mtwara kuunganishwa na Reli

25 March 2024, 17:26 pm

Kamati ya Bunge ya kudumu ya Bunge ya  uwekezaji wa mitaji ya umma wakiwa katika eneo la Gati jipya katika Bandari ya Mtwara.(picha na Musa Mtepa)

Changamoto zinazoikabili Bandari ya Mtwara ni kutokuunganishwa na miundombinu ya Reli pamoja na Barabara ya Mtwara –Dar es Salaam kutokuwa vizuri kuwezesha Bandari hiyo kuunganishwa na miundombinu  hiyo.

Na Musa Mtepa

Naibu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma Kijavala  amesema kuwa changamoto inayoikabili Bandari ya Mtwara  ni ukosefu wa kuunganishwa na miundo  ya Reli na Barabara hasa inayounganisha Mkoa wa Mtwara na Dar es saalam.

Hayo ameyasema leo 25/3/2024 kwenye ziara ya kamati ya Bunge ya kudumu ya uwekezaji wa mitaji ya umma ilipotembelea katika Bandari ya Mtwara kujionea uwekezaji  ulifanywa na Serikali ambapo Mhandisi Juma Kijavala amesema changamoto zinazo wakabili zipo nje ya mamlaka ya Bandari ikiwa ni pamoja na  kutokuunganishwa na miundombinu ya Reli pamoja na Barabara ya Mtwara –Dar es Salaam kutokuwa vizuri kuwezesha Bandari kuunganishwa na miundombinu  hizo.

Sauti ya Mhandisi Juma Kijavala naibu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

kwa upande wake mwenyekiti kamati ya Bunge ya kudumu ya  uwekezaji wa mitaji ya umma Deus Clement Sangu amesema kuwa wataendelea kuishawishi serikali iweze kuboresha miundo mbinu ya Barabara na Reli ili miradi hiyo iweze kuwa na tija kwa Wananchi wa mikoa ya kusini na serikali kwa ujumla. 

Sauti ya Deus Clement Sangu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya  uwekezaji wa mitaji ya umma

 Akizungumzia faida ya uwekezaji uliofanywa na serikali katika Bandari hiyo  Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda amesema kumekuwa na ajira  wanazozipata vijana na akina mama wa ndani na nje ya Mtwara kutokana na uwekezaji huo.

Sauti ya Mwanahamisi Munkunda mkuu wa wilaya ya Mtwara