Jamii FM

Wataalamu wa Elimu wafanya ufuatiliaji Mtwara Vijijini

25 February 2021, 06:35 am

Timu ya wataalamu ikiongozwa na Afisa elimu Msingi Mwl. Adam Shemnga Jana Tarehe 24 Februari, 2020 wamefanya ufuatiliaji na ukaguzi wa maendeleo ya kitaaluma katika Shule kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye Sekta hiyo Mtwara Vijijini.

Moja ya shule iliyotembelewa na wataalamu

Ukaguzi huo umelenga kufuatilia Hali ya ufundishaji, kiwango Cha kuelewa kwa Wanafunzi, uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu yaani KKK kwa Darasa la kwanza hadi la tatu, Maandalizi na mgawanyo wa idadi ya masomo na vipindi kwa Siku hadi wiki Pamoja na ukaguzi wa maendeleo ya Miradi inayotekelezwa kwenye baadhi ya Shule.

Zaidi ya hapo, wataalamu wa Sekta ya Elimu wetumia fursa hiyo Kusisitiza kuwasihi Walimu Kuimarisha Uhusiano na ushirikiano Kazini, kuheshimu Jamii wanayoishi nayo Pamoja na kuendelea kutumia lugha zenye staha kwa kipindi chote wanapotoa huduma kwa Jamii.

Aidha Afisa Elimu amewahakikishia Walimu kuwa ameanza kuzifanyia kazi changamoto zao zilizofika mezani kwake huku akiwataka kuendelea Kufanya Kazi kwa Kuzingatia miiko na Maadili ya Ualimu.

Juu ya hapo, Walimu Wakuu waliokaguliwa wameonesha furaha na kuahidi kutekeleza yote yaliyoagizwa kupitia majumuisho, timu ya wataalamu wa elimu imefanikiwa kufanya ufuatiliaji katika Shule ya msingi Tangazo, Kihimika, Mahurunga na Kilombero.

Credit: Afisa habari – Isaac Bilali