Jamii FM

Zahanati ya mbawala chini kufunguliwa leo

5 May 2021, 12:26 pm

Na Karim Faida

Mganga mkuu wa Manispaa ya Mtwara mikindani Dkt Joseph Kisala amesema leo Mei 5 2021 wanatarajia kufungua zahanati ya mtaa wa Mbawala chini iliyopo kwenye kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara mikindani mkoani Mtwara ili kuwarahisishia wananchi huduma hiyo ya Afya maana kwa saaa wanatumia Zahanati ya Naliendele.

Diwani Masudi Dali

Majibu hayo yametolewa baada ya Diwani wa Kata ya Naliendele ndani ya Manispaa hiyo Mh Masudi Dali kuhoji kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichafanyika Aprili 28 na 29. 2021 kuhusu lini Zahanati hiyo itafunguliwa maana wananchi wanatembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika maeneo tofauti.

Baraza la Madiwani la Manispaa katika kikao

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Mtwara mikindani Mh Zuhura Mikidadi amesema hakuna haja ya kusubili kwa kuwa watumishi wameshaandaliwa na vitendea kazi vipo tayari.

Zahanati ya Mbawala chini

Kufunguliwa kwa Zahanati hiyo itakuwa msaada kwa wananchi wa kijiji cha Nyengedi, Nanyati, mtaa wa Naulongo, na hata Mbawala chini penyewe na pia itasaidia kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika zahanati ya Naliendele Manispaa ya Mtwara mikindani.