Jamii FM

Mila, desturi  kikwazo  wanawake kushiriki nafasi za uongozi Mtwara

27 March 2024, 17:00 pm

Bi Rebecca Kisenha akifuatilia majadiliano ya wawakilishi wa vijana kutoka Mtwara vijijini juu ya mila zinazo mrudisha nyuma mwanamke katika kushiriki nafasi za uongozi(Picha na Musa Mtepa).

Mila na desturi potofu zimekuwa  zikiwarudisha nyuma wanawake wengi wilayani Mtwara kushiriki katika nafasi za uongozi na uamuzi na kupelekea kuwa wachache katika ushiriki kwenye vikao vya uamuzi.

Na Musa Mtepa

Imeelezwa kuwa mila na desturi  zinazofanyika katika jamii ndicho kikwazo kikubwa kwa wanawake wengi  wialayani Mtwara kutoshiriki katika nafasi za uchaguzi na uongozi  hali inayopelekea  kuwa wachache  katika vikao vya maamuzi.

Hayo yameelezwa 26/3/2024 na Bi Habiba Chiwalila mkazi wa kijiji cha Nanyati  Halmashauri ya wilaya Mtwara  mkoani Mtwara katika majadiliano ya mila na desturi  potofu zinazomrudisha nyuma mwanamke kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi yaliyoandaliwa na shirika la mtandao wa jinsia Tanzania TNGP ambapo amesema kuwa mfumo dume uliotapakaa katika jamii  nyingi unaomweka  mtoto wa kike nyuma ndio kikwazo kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi.

Sauti ya 1 Bi Habiba chiwalila mkazi wa Nanyati

Aidha Bi Habiba ameongeza kuwa kitendo cha Wanaume kuwaachia Wanawake majukumu mengi ya kuhudumia familia  kama vile kulea watoto,huduma za afya pamoja na huduma ya kuteka maji  huchangia Mwanamke kutoshiriki katika mikutano ya maamuzi inayofanyika katika vijiji.

Sauti ya 2 Bi Habiba chiwalila mkazi wa Nanyati

Kwa upande wake Shekhe Mvita Bin Musa mkazi wa kijiji  cha Kawawa  amesema kuwa karibia Dini zote zina ruhusu mtoto wa kike kuwa kiongozi huku akitoa tahadhari ya kuwa Mwanamke ameumbwa kuwa dhaifu hiyvyo ni rahisi kushawishika  akiwa kiongozi.

Sauti ya  1 Shehe Mvita Bin Musa Mkazi wa kijiji Cha Kawawa.

Pia Shehe Mvita amesema kuwa ili kuondoa changamoto ya kutojiamini na kutoshiriki katika nafasi za uongozi na uamuzi ni vema jamii ikawekeza katika Elimu kwa mtoto wa kike.

Sauti ya 2 Shehe Mvita Bin Musa Mkazi wa kijiji Cha Kawawa.

Naye Bi Rebecca Kisenha Mwezeshaji  kutoka shirika la Mtandao wa jinsia Tanzania TNGP amesema kuwa  jamii haina budi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo zimekuwa zikileta matokeo hasi kwa mtoto wa kike katika kufikia malengo  yake katika Elimu pamoja na kutoshiriki katika kupigania nafasi za uchaguzi ,uongozi na maamuzi.