Jamii FM

VIKUNDI 52 KUKOPESHWA MILIONI 205 MTWARA

9 July 2021, 16:30 pm

Na Karim Faida.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ndugu Dunstan Kyobya akizungumza katika hafla hiyo

Jumla ya vikundi 52 kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, wamepewa mkopo wenye thamani ya Tsh 205,047,000.

Juliana Manyama, Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Mtwara mikindani

Hayo yametanabaishwa na Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Mtwara mikindani mkoani hapa Bi Juliana Manyama jana katika hafla fupi iliyofanyika jana Julai 8 katika viwanja vya Mashujaa Park Mtwara.

Mfano wa hundi

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mtwara na mgeni rasmi katika hafla hiyo Ndugu Dunstan Kyobya amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mtaa kusimamia vikundi vyao ili kuhakikisha mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati na kuwataka wale wote ambao hawajarejesha mikopo mbalimbali hatua za kisheria zichukuliwe juu yao.

Bajaji aliyokopeshwa Ndugu Francis Chiwango

Nae Francis Chiwango ambae ni mtu mwenye ulemavu wa mguu, ni mmoja kati ya wanufaika ambae amekopeshwa Bajaji yenye thamani ya Tsh 7950,000. Ndugu Chiwango ameishukuru Manispaa hiyo kwa kukubali kumkopesha Bajaji hiyo huku akiahidi kurudisha mkopo huo kwa wakati.

baadhi ya wanawake wakiwa kwenye hafla hiyo

Kati ya vikundi hivyo 52, vikundi 39 ni vya wanawake, watu wenye ulemavu wapo 8 na vikundi 5 vya vijana.