Jamii FM

Makala ya udumavu kwa watoto chini ya miaka 8

9 May 2024, 17:45 pm

Baadhi ya watoto wa wilaya ya Nanyumbu wakiwa kwenye uzinduzi wa programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendelelo ya awali ya mtoto. Picha na Gregory Milanzi

Makala haya yanalenga kutoa elimu ya udumavu na wazazi kutakiwa kuzingatia mlo kamili ili watoto waweze kukua wakiwa na afya iliyo njema

Na Gregory Milanzi, Mwanahamisi Chikambu

Ni kipindi kinaelezea hali ya udumavu katika wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwarax, tathimini ya hali ya lishe, iliyofanyika katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mtwara na jumla ya wanafunzi shule za msingi na darasa la awali, jumla ya wanafunzi 5,736 waliweza kufanyiwa tathmini kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2023.

Kupitia kipindi hiki utawasikia wananchi kutoka wilaya ya Nanyumbu, wanazungumzia vipi juu ya elimu ya udumvu pia utamsikia afisa lishe kutoka wilaya ya Nanyumbu ameeleza mikakati ya Halmshauri katika kuhakikisha wanatoa elimu ya udumavu na kupunguza idadi ya udumavu.

Wengine waliosikika ni Pamoja na mdao wa watoto na Mwezeshaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ngazi ya Mkoa Mtwara

Bonyeza hapa kusikiliza