Jamii FM

Tume ya Haki za Binadamu watoa elimu

25 November 2021, 11:37 am

“Hatuwezi kufanya peke yetu tunajua kwamba Tume ni Taasisi huru ya Serikali lakini lazima tufanye kazi kwa pamoja kwahiyo ni wajibu wetu mkubwa kama alivyosema ndugu yangu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tuendelee kuelimisha ndugu zetu Wananchi kwenye maeneo mbalimbali lakini vile vile tuhakikishe kwamba tunafanya kazi kwa kushirikiana wote kwa pamoja”

Dkt. Fatma Halfani

Na Gregory Millanzi;

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekuja kutoa elimu kwa Wananchi Mkoani Mtwara ili waweze kutambua misingi mbalimbali ya Haki za Binadamu, Misingi ya Utawala Bora pamoja na Utu wa Mtu katika majukumu yao.

Hayo yameelezwa leo/jana na Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Fatma Halfan wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiwa kwenye picha ya Pamoja na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt Fatma Halfani baada ya kutembelea ofisi ya mkoa kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Ziara hiyo ina lengo la kubadilishana, kujadiliana na kukuza   elimu ya Utawala Bora na Haki za Binadamu kwa makundi mbalimbali ikiwemo Ofisi za  Serikali, Asasi za Kiraia, Mashuleni pamoja na Wananchi kwa ujumla.

Alisema Dira na dhamira ya Tume na Serikali kwa ujumla ni kuwa na Jamii yenye kuheshimu Haki za Binadamu Misingi ya Utawala Bora na Utu wa Mtu lakini pia kuongoza ukuzaji Ulinzi na uhifadhi wa Haki za Binadamu Misingi ya Utawala Bora Utu wa Mtu kwa kushirikana wote kwa pamoja.

“Hatuwezi kufanya peke yetu tunajua kwamba Tume ni Taasisi huru ya Serikali lakini lazima tufanye kazi kwa pamoja kwahiyo ni wajibu wetu mkubwa kama alivyosema ndugu yangu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tuendelee kuelimisha ndugu zetu Wananchi kwenye maeneo mbalimbali lakini vile vile tuhakikishe kwamba tunafanya kazi kwa kushirikiana wote kwa pamoja”,Alisema Halfan

Mkuu wa mkoa wa Mtwara katika picha ya pamoja

Alisema kuwa mpaka sasa tayari wana kilabu 254 mashuleni ambazo wamezianzisha kuanzia Shule za msingi mpaka Vyuo Vikuu nchini lengo likiwa ni kuwandaa wanafunzi hao ili waje kuwa viongozi wenye kuzingatia Haki za Binadamu Misingi ya Utawala Bora kwa kuzingatia Mila na Desturi kwa kuwa na Uzalendo na nchi yao.

Kwa uepande wake Mkuu wa Mkoa huyo wa Mtwara alisema kuwa Haki za Binadamu kwa namna moja ama nyingine zinawea kuathiriwa na Viongoizi katika kada mbalimbali kwahiyo ujio wa Tume hiyo kwenye ngazi za Wilaya na Mkoa ujmla ni hatua nzuri ya kukumbushana majukumu ya msingi yanayoweza kumuhudumia Mtanzania bila kuathiri haki zake lakini pia kuonyesha masuala la msingi ya Utawala Bora.

“Ni jambo la msingi sana ambalo mumelifanya niwapongeze Tume na niwaombe ziara hizi ziendelee sana na mpange mda wa kutosha katika Mamlaka zetu hizi za Mikoa ili tuweze kuwashirikisha Viongozi wengi katika Mamlaka zetu kadri itakavyowezekana ili tuweze kuwapa uelewa wa mambo ya msingi ya kuzingatia tunapohudumia Wananchi wa kawaida”,Alisema Gaguti

Hata hivyo Uongozi wa Mkoa huo kwa kupitia ziara hiyo wataendelea kuwakumbusha Wananchi utaratibu nzuri au mambo ya msingi ambayo wanatakiwa kujua kwani inawezekana kumekuwa na ukimya lakini bila kujua Watu wao wanaowaongoza hawana uelewa kuwa kitu ambacho wanastahili.

Alisema kuwa,  kupitia ngazi ya Tume Makao Makuu ni vema kukawa na vipindi vyenye kuelimisha Jamii na kupitia Viongozi hao katika vikao vyao wawe wawazi kwa wananchi kuwapa fursa ya kuwasikiliza ili kuweza kutambua changamoto zao na inapoonekana kuna mambo hayajakaa sawa hatua ziweze kuchukuliwa kwa wakati.