Jamii FM

Ushirika kuuza korosho kidijitali msimu huu

17 September 2023, 17:20 pm

Na Gregory Millanzi

Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) wanatarajia kuuza korosho kwa mfumo wa kidijitali kwa msimu wa mazao wa 2023/2024 mfumo ambao utatumia kompyuta kwenye kila chama cha ushirika cha msingi (AMCOS) na kutumia mizani ya kidijitali ili kuhakikisha mkulima anapata taarifa sahihi za kilo zake na kupata mapato sahihi.

Mrajis wa vyama vya ushirika Tanzania Dkt. Benson Ndege amesema wameamua kutumia mfumo huo ili kuhakikisha mkulima anapata taarifa sahihi ya mazao yake na kupata kipato sahihi cha mazao yake na mkulima anaweza kupata taarifa zake kupitia simu yake ya mkononi.

Sauti ya Dkt. Benson Ndege Mrajis wa vyama vya ushirika Tnzania

Jengo la ghala la mazao lilipo Mangaka Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, ambalo limezinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (Picha na Gregory Millanzi)

Meneja wa chama kikuu cha ushirika Mtwara (MAMCU) Biadia Matipa amesema wamepokea maagizo ya serikali na wamehaidi kuyafanyia kazi, na wanatarajioa kuanza kutumia  mfumo huo kwa msimu huu wa korosho.

Sauti ya Biadia Matipa Meneja wa MAMCU

Pia Biadia Matipa amesema kuwa wameshajiandaa kuhakikisha wanatoa elimu kwa viongozi wa AMCOS kuhusu mfumo mpya wa kidigitali .

Sauti ya Biadia Matipa Meneja wa MAMCU

Hayo yamezungumzwa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kwenye ziara ya Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani wakati akifungua ghala la mazao.