Jamii FM

RC Gaguti: Wanamtwara tujitokeze kesho kwenye uwanja wa Mashujaa

5 March 2022, 17:00 pm

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti kwa kushirikiana na taasisi ya “Bega kwa Bega na Mama” imewaomba wanamtwara kujitokeza kwa wingi siku ya kesho tarehe 06/03/2022 katika kusherehekea mwaka mmoja kwa serikali ya awamu ya sita katika uwanja wa wa mashujaa.Hamasa hii inatokana na maombi ya vijana wa mtwara hasa Bodaboda, wamachinga, na wajasiliamali wadogowadogo wa mtwara kuhitaji kushurehekea mafanikio ya mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri jeshi mkuu Mh. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mkuu wa mkoa mtwara amesema Baada ya maadhimsho hayo yatafuatiwa na shughuli mbalimbali zitakazodumu kwa zaidi ya wiki moja huku matukio mbalimbali yakiendelea kufanyika ndani ya mkoa wa Mtwara.

Msikiliza Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti akizungumza na waandishi wa Habari