Jamii FM

TANESCO Mtwara yachapwa goli 3-1 na Veteran Mtwara

27 February 2021, 11:23 am

Timu ya shirika la umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Mtwara, wamechapwa goli 3-1 na timu ya Veteran Mtwara.

TANESCO na timu ya Veteran katika michezo mbalimbali

Mechi hiyo ya mpira wa miguu iliyochezwa leo februari 27, 2021 kwenye viwanja vya bonanza mkoani hapa, TANESCO wamefungwa goli zote tatu katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kipindi cha pili timu zote zilianza kwa kushambuliana na dakika ya 79 ya mchezo timu ya Tanesco wakapata goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa adhabu ndogo iliyopigwa nje ya 18 na kufanya matokeo mpaka mwisho ni 3 kwa 1.

Mechi hiyo ilikuwa ni sehemu ya bonanza ambalo limeandaliwa na TANESCO Mtwara kwa ajili ya kuaga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka 2021.

Michezo mingine iliyochezwa ni kuvuta kamba kati ya mashabiki wa Yanga na Simba ambao ni wafanyakazi wa TANESCO, kukimbia na yai kwenye kijiko, kukimbia na magunia, mbio fupi kwa wanawake na wanaume na kukimbiza kuku.

Credit: Gregory Millanzi

Matukio katika picha

Wafanyakazi wa TANESCO Mtwara wakicheza michezo wa kuvuta kamba