Mkurugenzi mtendaji wa Jamii FM Radio akihojiwa na Grace Hamisi katika studio ndogo za Jamii FM. Picha na AMua Rushita
Jamii FM

Mahitaji ya kupata habari ni makubwa kwa sasa – Said Swallah

13 February 2024, 11:30 am

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii FM Radio akihojiwa na Grace Hamisi katika studio ndogo za Jamii FM. Picha na AMua Rushita
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii FM Radio Ndugu Said Swallah akihojiwa na Grace Hamisi katika studio ndogo za Jamii FM zilizopo Madukani Mkoani Mtwara. Picha na Amua Rushita

Na Grace Hamisi, Amua Rushita

Kila ifikapo Februari 13 ya kila mwaka  dunia huadhimisha siku ya Redio Duniani ambapo huzungumziwa mchango wa redio katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo, changamoto wanazokutanazo jamii na kuziwasilisha kwa wenye mamlaka .

Lakini pia redio imekuwa ikitengeneza urafiki na umoja baina ya watu katika jamii, katika kuelekea maadhimisho hayo Jamii FM Radio imepata nafasi ya kuzungumza na mkurugenzi mtendaji wa  Jamii FM Ndugu Said Swallah ambapo ameelezea umuhimu wa redio pamoja na sababu za kuanzishwa kwa kituo hiki cha habari kwa mkoa wa Mtwara.

Swallah amesema “Kinachotolewa redioni kinagusa makundi mbalimbali, kasi imeongezeka ya uanzishwaji wa redio na pia maudhui yamekuwa na mabadiliko makubwa, kinachojitokeza ni kuwa mahitaji ya kupata habari ni makubwa kwa sasa na hii imetokana na dunia kuwa kijiji”

“Mtu anaweza kuwa kijijini lakini akawa anafuatilia habari za mataifa mengine yaliyo nje ya eneo lake”. ameongezea Swallah

Karibu usikilize mahojiano haya juu ya siku ya redio duniani

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii FM Ndugu Said Swallah akizungumzia umuhimu wa redio ya jamii katika siku ya redio duniani 2024