Jamii FM

Dangote kuanza uzalishaji tena Jumatatu 11.01.2021

10 January 2021, 06:53 am

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mh. Gelasius Byakanwa katika kiwanda cha Dangote Cement.

Uongozi wa kiwanda cha Saruji DANGOTE CEMENT Mtwara umesema jumatatu ya Januari 11, 2021 wataanza uzalishaji wa Saruji baada ya kukamilika kwa matengenezo ya baadhi ya mitambo iliyopata itirafu.

Hayo yamethitishwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mh. Gelasius Byakanwa alipotembelea kiwandani hapo na kujionea matengenezo yanayoendelea kwenye baadhi ya mitambo katika kiwanda hicho.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mtwara Mh. Gelasius Byakanwa

Nae Mkurugenzi mkuu wa Dangote Cement Mtwara Abdullah Ababa amemshukuru Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya Mtwara kwa kuendelea kuwasihi wafanyabiashara kuacha kuongeza bei ya bidhaa ya Saruji sokoni.

Sauti ya Mkurugenzi mkuu wa Dangote Cement Mtwara