Jamii FM

Binti mwenye ulemavu atuhumiwa kujinyonga hadi kufa

14 September 2023, 06:58 am

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ACP Mtaki N Kurwijila akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Picha na Musa Mtepa

Marehemu amekutwa amefungwa kamba aina ya Manila shingoni huku puani akichuruzika Damu.

Na Musa Mtepa

Katika hali isiyo ya kawaida Samia Ahmad Mohamed (20), mkazi wa kijiji cha Sinde, Msangamkuu Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, mlemavu wa mikono na miguu amekutwa amefariki Dunia nyumbani kwake huku mwili wake ukiwa unavuja damu puani na mdomoni.

Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa kijiji cha Sinde kilichopo kata ya Msangamkuu Abdukarim Asilia amesema kuwa kwa taarifa alizopata kutoka kwa wananchi kuwa mtoto huyo amekutwa amejinyonga huku akisubiri taarifa kamili kutoka kwa Jeshi la polisi juu ya tukio hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa kijiji cha Sinde kilichopo kata ya Msangamkuu Abdukarim Asilia

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo September 11 ,2023 kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ACP Mtaki N Kurwijila amesema kuwa marehemu amekutwa amefungwa kamba aina ya Manila shingoni huku puani akichuruzika Damu.

Sauti ya kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ACP Mtaki N Kurwijila

Kwa upande wa Baba mzazi wa Marehemu huyo Bw Ahmadi Idd Ahmad amesema kuwa alipata taarifa ya kifo cha Mtoto wake baada ya kupigiwa simu na mke wake akiwa anatokea baharini kuwa Samia amekutwa amefariki pembezoni mwa uwani huku shingoni akiwa amefungwa kamba.

Sauti ya Baba mzazi wa Marehemu Bw Ahmadi Idd Ahmad

Kwa upande wa Diwani wa kata ya msangamkuu Hamisi Mangorosho amesema kuwa yeye kama kiongozi amepokea kwa hudhuni tukio hilo huku akiwataka wananchi kuwa karibu na watu wenye ulemavu ili kuwapunguzia mawazo wanayokuwa nayo.

Sauti ya Diwani wa kata ya msangamkuu Hamisi Mangorosho