Jamii FM

Wanafunzi 11 na watu wazima 2 Wafariki katika ajali ya Basi la wanafunzi la King David Mtwara

26 July 2022, 20:37 pm

Na Gregory Millanzi.

Kufuatia ajali ya Basi dogo la Wanafunzi aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T207 CTS la shule ya King David Mtwara imepata ajali eneo la Mji mwema Kata ya Magengeni, Mikindani Mkoani Mtwara Wanafunzi 11, Dereva na mwangalizi Wamefariki na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 13.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo, amethibitisha kuwa wanafunzi 11 wamefariki na watu wazima 2 ambao walikuwa kwenye basi hilo la shule.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt Mohamed Nyembea amethibitisha kupokea majeruhi 17 ambao 12 ni wakike na 6 ni wakiume na waliofariki 13.

“Asubuhi ya leo tumepokea wagonjwa ambao wameletwa hapa baada ya kutokea ajali na katika ajali hiyo, Tumepokea majeruhi 17, kati yao 12 ni wakike na 6 ni wakiume, na kumetokea vifo Jumla watu 13, watoto wako 9 wasichana 6 na wakiume 3 na watu wazima 2 ambao ni mwanaume na mwanamke” amesema Dkt Nyembea.

Pia Dkt Nyembea ameongea kuwa kuna wagonjwa 5 ambao hali zao ni Mahututi sana na wanaendelea kuwapatia matibabu ili kunusuru maisha yao.

Miili ya Wanafunzi hao imeagwa leo saa tisa Alasiri katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula Mkoani Mtwara.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.