Jamii FM

Vifo vya wajawazito, watoto wachanga bado ni changamoto Mtwara-Makala

23 December 2023, 15:21 pm

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara mjini. Picha kwa msaada wa mtandao

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu mkoa wa Mtwara, kumekuwepo na ongezeko la vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kwa kipindi cha miezi mitatu.

Na Gregory Millanzi

Binadamu tunapitia nyakati tofauti tofauti katika maisha yetu, baadhi ya nyakati tunazopita ni FURAHA na HUZUNI.

Furaha mojawapo tunayopitia kwenye maisha ni pale Baba  na Mama wanapojaliwa kupata mtoto na kuongeza familia, hili ni tukio la furaha sana kwa familia pamoja na ndugu na jamaaa.

Baba mmoja wa familia ambaye amekaa nje ya kituo cha afya akiwa na furaha hasa anapopata taarifa kuwa mkewe yupo wodi ya mama wajawazito akiendelea na huduma ya kujifungua, na wakati mwingine akiwaza atapokeaje taarifa ya kupata mtoto wa kiume au wa kike.

Wakati akiendelea kusubiri nje ya jengo hilo akiwa na hamu kubwa ya kuitwa baba kwa mara ya kwanza, mara anatokea Daktari akiwa na masikitiko makubwa na kumwambia maneno ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake.

Kusikiliza Makala haya Bonyeza Hapa