Jamii FM

RPC Mtwara: Zingatieni sheria za usalama barabarani

10 April 2024, 23:17 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Swala ya Eid Al-fitri katika viwanja vya Sabasaba mjini Mtwara (Picha na Musa Mtepa)

kKuvaa kofia ngumu kwa mwendesha wa pikiki ni suala la kisheria hivyo ni wajibu kwa maafisa usafirishaji (Bodaboda) wote mkoani Mtwara na abiria wake kuzingatia sheria hiyo.

Na Musa Mtepa

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Issa Suleimani amewataka maafisa usafirishaji (Bodaboda) na watumiaji wa  vyombo vya moto barabarani  kutii sheria bila shuruti  ili kupumguza ajali zisizo na ulazima.

Wito huo ameutoa leo 10/4/2024 baada ya Ibaada ya Eid el-Fitir iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba mjini Mtwara ambapo amesema kuwa kuvaa kofia ngumu kwa mwendeshaji wa Pikiki ni suala la kisheria hivyo ni wajibu kwa maafisa usafirishaji (Bodaboda) wote mkoani Mtwara yeye na abiria wake kuzingatia sheria.

Sauti ya 1 SACP Issa Suleiman kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara

Pia Kamanda wa polisi amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika kipindi hiki cha sikukuu umeimarika  katika sehemu zote  za mkoa wa Mtwara huku akiwataka Wananchi wanapotoka Kwenda matembezi wasitoke watu wote na nyumba kuiacha bila uwepo wa mtu wa kuilinda.

Sauti ya 2  SACP Issa Suleiman kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara