Jamii FM

Taharuki ujenzi wa shule Namkapi watatuliwa

5 July 2023, 15:28 pm

Kibao Cha shule ya msingi Namkapi. Picha na Musa Mtepa

Wananchi wa Kijiji cha Namkapi wamepatwa na hofu baada ya kupata tetesi za kuhamishwa kwa shughuli za ujenzi wa shule, Jamii FM imefuatilia kwa undani juu ya taarifa hizo

Na: Musa Mtepa

Wananchi wa kijiji cha Namkapi, kata ya Dihimba Halmashauri ya Mtwara vijijini wameilalamikia Serikali ya wilaya kwa kitendo cha kuondoa baadhi ya majengo ya shule ya msingi yaliyokusudiwa kujengwa katika kijiji hicho.

Mwandishi wa Jamii FM Musa Mtepa alizungumza na mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Namkapi

Wakizungumza na Jamii fm Radio wananchi hao wamesema kuwa awali walipewa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa na jengo la utawala hali iliyowahamasisha kuwekeza nguvu zao katika ujenzi huo kwa kuchimba msingi na shughuli nyinginezo.lakini kwa hivi sasa hali imekuwa tofauti baada ya kupata taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya vyumba vya Madarasa na kupelekwa eneo lingine.

Sauti za wananchi wa kijiji cha Namkapi

Bi Somoe Athumani ambaye ni mama wa watoto wanaosoma eneo tofauti na kijiji hicho ameelezea kusikitishwa kwake kwa kitendo cha kupunguza vyumba vya madarasa hayo akihitaji sababu ya kuondoa vyumba hivyo kupeleka kijiji kingine huku akielezea athari wanazopata watoto wanaosoma umbali mrefu kutoka kijijini hapo.

Sauti ya Bi. Somoe Athumani

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Mtwara Hanafi Msabaha ametoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo kwa kuwatoa hofu wananchi hao kuwa shule hiyo itajengwa na itakamilika na kuahidi kila mwaka halmashauri itakuwa inajenga majengo mawili ili ikamilishe idadi ya vyumba vya madarasa tisa vilivyopangwa hapo awali.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Hanafi Msabaha