Jamii FM

Tunaomba barabara ikamilike

21 May 2021, 04:58 am

Na Karim Faida

Wananchi wa Mtaa wa Kagera kata ya Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa wameiomba serikali kuwawekea kifusi kwenye Karavati lililojengwa na kukamilika katika barabara itokayo Stendi kuu ya Mabasi Mkoa wa Mtwara Chipuputa, na kutokezea kwenye kituo cha daladala cha Mnjaleni.

mwonekano wa eneo lenyewe la barabara

Wakiongea na Jamii fm radio kwa nyakati tofauti Madereva bodaboda wa stendi hiyo, Madereva Bajaji na hata wafanyabiashara wanaopatikana kandokando ya barabara hiyo, wamesema kutokana na kuwepo kwa karavati lililochomoza juu ya ardhi, limesababisha kufungwa kwa barabara hiyo kwa miezi mitatu sasa hivyo mambo yote ya maendeleo yanayotegemea barabara hiyo yamejifunga.

Meneja wa TARURA Manispaa, ya Mtwara Mikindani, Hatibu Nunu

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Manispaa ya Mtwara Mikindani Ndugu Hatibu Nunu amesema lengo la kuweka Karavati hilo ni kuyaondoa maji yaliyokuwa yakituwama katika eneo hilo na ameahidi kama TARURA watahakikisha wanaweka kifusi ndani ya siku 14 ili ipitike kama kawaida.