Jamii FM

Viongozi, wapeni ushirikiano waandishi wa habari

3 May 2021, 12:40 pm

Na Karim Faida

Waandishi wa habari mkoa wa Mtwara wamekuwa wakikosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali pale wanapohitaji Kuweka mizania ya habari zao huku sababu ikiwa ni kuhofia kupoteza nafasi zao za kazi.

Patrick Kyaruzi ambae ni mgeni rasmi

Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa Tiffany Diamond hapa mkoani Mtwara na Ndugu Patrick Kyaruzi ambae ni mgeni rasmi na Mchumi wa mkoa wa Mtwara akimwakilisha Afisa maendeleo ya jamii wa Mtwara mikindani katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.

Waandishi wa Habari na Wadau mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya vyombo vya Habari Duniani

Hata hivyo Kyaruzi ambae kitaaluma ni Mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara amesema ili kuienzi siku kama ya leo ni lazima waandishi wapate ushirikiano ili kuendelea kufanya kazi zao kwa uhuru.

Pia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwawezesha waandishi wao kifedha na usafiri pale wanapokuwa kwenye majukumu yao ili waweze kutoa habari za kweli na sio kuwapamba watu.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Shirika la We World chini ya mradi wao wa Sauti Mpya.