Jamii FM

Manispaa ya Mtwara yapitisha makisio ya bajeti ya sh Bil 30.1 kwa mwaka 2022/2023

3 February 2023, 21:55 pm

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani wakifatilia kikao cha baraza la Madiwani la Bajeti lilifanyika Februari 3, 2023 (Picha na Gregory Millanzi).

Baraza la madiwani Manispaa ya Mtwara Mikindani, limepitisha makisio ya bajeti ya shilingi Bilioni 30.1 kwa mwaka 2022/2023.

Na Gregory Millanzi.

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani mkoani Mtwara wameridhia kupitisha bajeti ya shilingi Bilioni 30.132 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 ambayo itatumika katika miradi mbalimbali za kimaendeleo.

Mkuu wa idara ya mipango na uratibu Manispaa ya Mtwara Mikindani Bw Gwakisa Mwasyeba, akisoma makisio ya bajeti ya mwaka 2022/2023 (Picha na Gregory Millanzi).

Akiwasilisha mchanganuo wa bajeti leo Februari 3,2023 katika kikao maalumu cha kupitisha mpango wa bajeti ya halmashauri, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Bwn. Gwakisa Mwasyega ameeleza fedha hizo zitatokana na vyanzo vya ndani vya mapato ambavyo vitachangia shilingi Bilioni 5,445,000,000, Ruzuku ya matumizi mengineyo milioni 840,688,200.

Aidha kwa upande wa Ruzuku ya mishahara itachangia bilioni 15,792,162,200, Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikalini bilioni 5,627,920,497 na Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka kwa Wahisani bilioni 2,426,500,506.

Katika utekelezaji wa bajeti hiyo umejielekeza kwenye vipaumbele vya kusimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato, uboreshaji wa mapato, uboreshaji wa upatikanaji wa huduma zenye ubora kwa jamii na kadhalika.