Jamii FM

Maji bonde la Ruvuma, Pwani ya Kusini ni stahimilivu kwa wananchi

19 April 2024, 21:14 pm

mwonekano wa juu wa mto na bonde la ruvuma (picha kwa msaada wa mtandao)

Bonde limefanya tathmini ya maji yaliyopo juu ya ardhi na chini ya ardhi na linavituo vya kufuatilia mienendo ya maji na tunatoa vibari kwa wahitaji wa matumizi ya maji hasa kwa wanaohitaji kuweka miundombinu.

Na Musa Mtepa

Jumla  ya vyanzo vya maji 81 vimeainishwa kwa ajili ya kuhifadhi  ambavyo vina miradi mikubwa ya usambazaji wa  maji kwa jamii katika mkoa wa Mtwara.

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini Bw Jaribu Modest Liana alipokuwa akizungumza na Jamii fm Radio ambapo amaesema kuwa bonde limeainisha jumla ya vyanzo 81 vinavyo jumuisha miradi mikubwa inayotumiwa na wananchi katika mkoa Mtwara.

Sauti ya 1 Jaribu Modest  kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji ya bonde la Ruvuma na pwani ya kuisni

Aidha Bw Modest amesema kuwa rasilimali ya maji iliyopo kwenye bonde la Ruvuma na pwani ya kusini ni zaidi ya mita za ujazo milioni 14.09 ambazo ukilinganisha na idadi ya watu waliopo katika bonde kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika  Mwaka 2022 kwa mkoa wa Mtwara ina jumla ya watu zaidi ya milioni 4.67 hivyo mahitaji ya maji kwa watu kwa kuzingati mizania ya kimataifa  ni stahimilivu.

Sauti ya 2 Jaribu Modest  kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji ya bonde la Ruvuma na pwani ya kuisni

Pia Bw Modest Liana amesema kuwa moja ya jukumu kubwa linalofanywa na ofisi ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini ni kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinatunzwa na kuhifadhiwa ili viwe endelevu  kwa mahitaji ya sasa na ya baadae.

Sauti ya 3 Jaribu Modest  kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji ya bonde la Ruvuma na pwani ya kuisni

Kwa mujibu wa ofisi ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini inaelezwa kuwa zaidi ya lita za ujazo milioni 14.09  zipo katika bonde  hilo huku ikielezwa kuwa lita za ujazo milioni 11.097 ni vyanzo vinavyopatika juu ya ardhi kama vile mito,chem chem, ziwa na mabwawa na  lita za ujazo milioni 3.023 zinapatikana chini ya Ardhi .