Jamii FM

Wasanii Mtwara kuchangamkia fursa

9 August 2023, 17:43 pm

Wasanii wa Mkoa wa Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mtwara

Na Msafiri Kipila

Serikali imeendelea kuwawezesha na kutoa mafunzo kwa wasanii mkoani MtwaraAgosti 07, 2023 katika Ukumbi Wa TTC Kawaida hapa Mtwara, ili wasanii wapate mikopo na kujiajiri, kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na kuchangia pato la taifa. Katika mwaka 2023/24 Kutoka kwenye mfuko wa mikopo wa utamaduni na sanaa.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Hanaf Msabaha akizungumza na wasanii

Mkuu wa wilaya ya Mtwara ndugu Anafi Hasani Msabaha amewataka wasanii hao kuitumia fursa hiyo ili wasanii waweze kufaidika na pesa hizo 20 Bilioni na kuwasihi wazimitumie kwa matumizi sahihi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Ndugu Anafi Msabaha

Nyakaho Mtuli Mahemba Ni Mtendaji mkuu wa mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania, amesema mfuko huo umejikita zaidi katika kutoa huduma kwa wadau hususani wasanii waweze mujikwamua kiuchumi waweze kufanya kazi za sanaa kwa wepesi.

Sauti ya Nyakaho Mtuli Mahemba

Baadhi ya wasanii wamezungumza na kutoa shukrani kwa serikali kwa kuwaona na kuja na mikopo itakayowasaidia katika kazi zao lakini pia wameiomba serikali kuzingatia kulingana na wasanii wenyewe ili waweze kupata mikopo hiyo kwa urahisi.

Sauti ya Said Chande