Jamii FM

Rushwa ya ngono isichukuliwe kawaida

3 November 2023, 17:54 pm

Afisa Mipango na utawala kutoka shirika lisilo la kiserikali la Door of Hop Tanzania Bi Jesca Muhagama. Picha na Musa Mtepa

Rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi kwa upande mwingine ni suala la mkanganyiko kwa sababu ni suala Mtambuka huku akisema kuwa inawezekana Bosi akampenda kweli mfanyakazi wake lakini wakati mwingine anaweza kutafsiriwa kuwa ni Rushwa ya ngono

Na Musa Mtepa

Watanzania wameshauriwa kutochukulia kawaida suala la rushwa ya ngono kutokana na kuleta athari kubwa katika jamii ikiwepo magonjwa na wakati mwingine kupelekea hata kifo.

Akizungumza na Jamii Fm Radio Afisa Mipango na utawala kutoka shirika lisilo la kiserikali la Door of Hope Tanzania Bi Jesca Muhagama amesema kuwa jamii ya Mtwara na Taifa kwa ujumla wasichukulie kuwa kitu cha kawaida, wanatakiwa kuona kuwa ni kitu hatarishi kwasababu kimekuwa kikipelekea magonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo.

Sauti ya Bi Jesca Muhagama – Shirika la Door of Hope

Aidha Jesca amesema kuwa Rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi kwa upande mwingine ni suala la mkanganyiko kwa sababu ni suala Mtambuka huku akisema kuwa inawezekana Bosi akampenda kweli mfanyakazi wake lakini wakati mwingine anaweza kutafsiriwa kuwa ni Rushwa ya ngono hivyo jamii wanapasa kutofautisha kati ya Rushwa ya ngono na mapenzi ya kawaida kwa mfanyakazi.

Sauti ya Bi Jesca Muhagama – Shirika la Door of Hope

Kwa upande wake Bi Salima Katulituli mkazi wa Msangamkuu ambae pia ni Kungwi amesema kuwa wamekuwa wakihamasisha na kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia ikiwemo Suala kujihadhari na Rushwa la Ngono Mashuleni na Makazini.

Sauti ya Bi Salima Katulituli mkazi wa Msangamkuu