Jamii FM

Tunajenga chuo cha Mafuta, Gesi na Umeme ili kuwajengea uwezo watu wetu

28 November 2022, 14:54 pm

Waziri January Makamba (picha na mtandao)

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akiwa kwenye utiaji saini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) kitalu cha Ruvuma – Mtwara, Waziri Makamba amesema >> ‘Ndugu zangu wa Lindi na MTWARA – sasa nchi yetu inaanza kuingia kwenye uchumi wa gesi. Sio kwa tukio hili la leo tu, lakini kwa mlolongo wa matukio na jitihada za Serikali. Kule Arusha, tupo kwenye hatua za mwisho za majadiliano kwenye ule mradi wetu wa kuchakata gesi utakao gharimu zaidi ya trilioni 70. Huu utakuwa uwekezaji mkubwa barani Afrika.’ – Waziri Makamba

 

‘Pia eneo la Lindi, serikali imeamua kujenga Chuo (Polytechnic) cha mambo ya Mafuta, Gesi na Umeme, ili kujengie watu wetu uwezo’ – Waziri Makamba

 

‘Lakini pia tutajenga Special Economic Zone ndani ya eneo la mradi ili kuchochea maendeleo ya Lindi na Mtwara baada ya mradi kukamilika’ – Waziri Makamba