Jamii FM

Asasi za kiraia za paza sauti uchaguzi Mkuu

19 October 2020, 11:08 am

Asasi za kiraia zimetoa tamko la kulaani vitendo vya ukandamizaji, uonevu na udhalilishaji kwa wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali za uwakilishi ngazi ya ubunge na udiwani.

Door of hope Tanzania, Mtwangonet, Fawopa na Nerio za mkoani Mtwara wanapinga vitendo vya udhalilishaji, uonevu na ukandamizaji kwenye kampeni za uchaguzi zinazoendelea kuelekea kilele chat siku yakupiga kura tarehe 28 oktoba 2020.

Wakizungumza kwa pamoja, wakurugenzi na watendaji wa asasi hizo Fidea luanda (Mtwangonet), Clemence Mwombeki(Door of hope Tanzania) Judith Chitanda (Nerio) na Baltazar Komba( Fawopa) wameeleza zaidi kupitia Jamii Fm Radio.