Jamii FM

TCCIA Mtwara kufanya uchaguzi leo

8 April 2021, 12:44 pm

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara, Viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Mtwara Swallah Said Swallah amesema hotuba ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hasan imerudisha matumaini kwa wakulima, Wafanyabiashara, na wenye viwanda mkoani hapa.

Swallah Said Swallah akizungumza katika mkutano huo

Amesema hayo leo April 8, 2021 katika ukumbi wa Tiffany Diamond hapa mkoani Mtwara katika mkutano wa 30 wa Chemba hiyo wenye lengo la kuwachagua viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amewataka viongozi watakaoshika nyadhifa hiyo leo kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi kama Pass ambao wanajihusisha na Kilimo, Uvuvi na biashara kwa maendeleo ya wanachama na wananchi wa Mtwara.

Dunstan Kyobya Mkuu wa wilaya ya Mtwara

Nae Mkuu wa mkoa wa Mtwara na mgeni rasmi katika mkutano huo Gelasius Byakanwa amewataka viongozi wapya kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hasan, kwa kuwapa ushirikiano wawekezaji kwa maslahi ya Wanamtwara.

Mkuu wa Mkoa Mtwara Gelasius Byakanwa

Chama cha wafanyabiashara, Viwanda na kilimo TCCIA kimeanzishwa mwaka 1989 huku Wanachama kutoka wilaya ya Newala, Tandahimba, Masasi, Nanyumbu na Mtwara Mjini wamehudhuria mkutano huo.