Jamii FM

Ngedere na Tumbili wavuruga shughuli za kilimo

11 February 2022, 11:53 am

Wanyama pori (Tumbili na Ngedere) wamekuwa kikwazo kwa wananchi  kufanya shughuli   za kilimo  kwa ufasaha  kwa baadhi ya kata za Halmashauri  ya Mtwara vijijini hali inayopekea  kukatamaa na shughuli  hizo.

Kikao cha Madiwani wakiwa wanaendelea na kikao

Akichangia Taarifa ya kamati ya uchumi ,ujenzi na Mazingira  Diwani wa Kata ya Ndumbwe  Mh Abdully Mahupa  kwenye kikao cha Madiwani kilichofanyika Februari 8, 2022 kwenye  ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Mustafa Sabodo ameiomba kamati hiyo kutengeneza  njia mzuri ya kuwasaidia  wananchi kuwazuia wanyama hao.

Mh Abduly Mahupa akizungumzia mahitaji ya mipango na mikakati

Akizitaja kata zinazo athiriwa na wanyama hao kuwa ni pamoja na Kata ya Ndumbwe, kata ya muungano,Mpapura na kata ya Libobe .

Mh Abduly Mahupa ameeleza wanyama hao kusumbua katika kata ya Ndumbwe na Kitele

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi  Maisha Mtipa  amesema kuwa wao kama  Halmashauri  watazungumza na wataalamu wa wanyamapori  ili kutembelea kata hizo waweze kuona namna ya kuwadhibiti  wanyama hao.

Kaimu Mkurugemzi Mh. Maisha Mtipa akifafanua mipango ya ya kukabiliana na wanya hao