Jamii FM

Waislam watakiwa kuishi maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu

10 April 2024, 13:52 pm

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika ibada ya Eid Fitir katika viwanja vya Sabasaba mjini Mtwara(picha na Musa Mtepa)

Kumewa na kutozingatia matukufu na makatazo ya Mwenyezimungu ambayo huenda ikawa sababu ya kuwepo kwa ugumu wa Maisha kutokana na Binadamu kutozingatia maagizo yake

Na Musa Mtepa

Waislam wametakiwa kuendelea kuishi Katika Maisha  walivyoishi kwenye  Mwezi mtukufu wa Radhamani ili kuendelea kumpendeza Mwenyezi Mungu na kuachana na vitendo vinavyo mchukiza .

Akihutubia Umma wa kiislamu uliojitokeza kwenye Ibada ya Eid fitir iliyofanyika Leo 10/4/2024  katika Viwanja vya Sabasaba Mjini Mtwara  Khatwibu Ustadhi Mohamedi Salumu  amesema  kumewa na kutozingatia matukufu na makatazo ya Mwenyezimungu ambayo huenda ikawa sababu ya kuwepo kwa ugumu wa Maisha kutokana na Binadamu kutozingatia maagizo yake.

Sauti ya 1 Ustadhi Mohamedi Salumu

Aidha Khatwibu Mohamedi amesema ili kuondokana na  Ugumu wa Maisha jamii haina budi kumrejea Mwenyez Mungu katika kutenda mema na kuachana na maovu.

Sauti ya 2 Ustadhi Mohamedi Salumu

Kwa upande Abdala Juma Muumini aliyejitokeza katika Ibada hiyo amewaomba Waislamu kuhakikisha ucha Mungu uliotafutwa kwenye Mwezi wa Ramadhani kuulinda kwa hima yote na kuishi katika Miezi iliyobakia kwa mtazamo huo ili kufikia kiwango cha Uchamungu.

Sauti ya Abdala Juma Muumini wa Dini ya kiislamu

Hata hivyo   katibu wa shura ya Maimamu  mkoa wa Mtwara Bakari Rashidi Mchira ametumia Ibada hiyo kutoa salamu kwa Serikali kuona haja ya kukaa na makampuni ya usafirishaji wa Makaay a Mawe kuzungumza na Madereva kuzingatia usalama wa watumiaji wengine wa Barabara ili kuondoa ajari zisizo na ualazima.

Sauti ya Bakari Rashidi Mchira  katibu wa Shura ya maimamu mkoa wa Mtwara