Wanawake wanabangua korosho
Jamii FM

Wanawake washauriwa kukuza kipato cha familia

31 January 2023, 12:07 pm

Bi Rabia Halidi Zuberi (kulia) akiwa na Shemsia Hamisi (Kushoto) wakiwa katika ubanguaji wa korosho, PICHA na Musa Mtepa

Wanawake wa Mkoani Mtwara wameshauriwa kupambana katika kutafuta  na kuongeza kipato cha familia  na kuachana na tabia ya kuwaacha wanaume pekee katika kutekeleza majukumu ya Nyumbani.

Na Mohamed Massanga

Akizungumza na Jamii fm Radio Mwenyekiti wa kikundi cha ‘’LIYAKAYA  WOMENI GROUP’’ kinachopataikana  Mtawanya juu mtaa wa  Zahanati Bi Rabia Halidi Zuberi  amewataka wanawake wenzake kujishughulisha na kazi mbalimbali katika kuiongezea familia kipato.

“Wanawake tusibweteke  kwa kukaa kusubiri wanaume kutuletea mahitaji ya nyumbani badala yake wapambane na kusaidia majukukumu ya wanaume majumbani.

“Wanawake tusibweteke  kwa kukaa kusubiri wanaume kutuletea mahitaji ya nyumbani badala yake wapambane na kusaidia majukukumu ya wanaume majumbani.”

Nao wanachama wa kikundi hicho wamesema kuwa kuna faida kubwa ya kuwa mwanakikundi kwani wamefanikiwa kuondoa changamoto za kifamilia kama vile mahitaji ya watoto ya shule  na mengineyo huku wakiomba pia  viongozi wa kata kuwa na utaratibu wa kutembelea vikundi vilivopo  kwenye maeneo yao utawala ili kujua changamoto wanazo pitia.