Jamii FM
Makala: Serikali na uboreshaji wa huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto
6 June 2024, 15:18 pm
Na Gregory Millanzi na Mwanahamisi Chikambu
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliwahi kulalamika kwenye makala zilizopita, kuhusu hali ya utolewaji wa huduma bora ya afya ya mama mjamzito na mtoto kwenye vituo vya afya na Hospitali, kuwa kuna baadhi wanadaiwa hela kwa ajili ya kuchangia huduma za afya.
Baada ya kusikia hayo, imepita miezi kadhaa tangu kutokea kwa changamoto hiyo ya Huduma ya Afya ya mama mjamzito na watoto chini ya miaka Mitano, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imeamua kuja na suluhisho la mpango wa mama na mwana. ungana na Gregory Millanzi na Mwanahamis Chikambu kwenye simulizi ya makala haya.