Afisa elimu Manispaa ya Mtwara Mikindani Nicolous Millanzi
Jamii FM

Wapelekeni watoto waanze darasa la awali na la kwanza

30 January 2023, 12:26 pm

Na Gregory Millanzi

Wazazi na walezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, wametakiwa kuwaandikisha watoto wenye umri wa miaka minne kwa ajili ya kuanza darasa la awali, na wenye umri wa miaka 6 kujiunga na darasa la kwanza  mwaka 2023.

Wito huo umetolewa wiki hii na Afisa elimu wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Nicolaus Millanzi, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Dira ya Asubuhi cha Jamii FM radio.

Afisa elimu amesema, wazazi na walezi wote wanatakiwa kuwaandikisha na kuwapeleka shule watoto wote wenye umri wa kuanza shule hasa darasa la awali na darasa la kwanza kwasababu Serikali imeweka miundombinu rafiki kwa ajili ya watoto kupata elimu.

Afisa Elimu wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Nicolous Millanzi akizungumza kwenye kipindi cha Dira ya asubuhi, Jamii FM Radio.

Ameongeza kuwa Serikali imeondoa ada kwa shule za msingi na sekondari, na pia wameongeza  madarasa kwenye baadhi ya shule na kuweka mazingira rafiki kwa watoto kusoma, kawahiyo wazazi na walezi wanapaswa kuwapeleka watoto wao kwenye shule za serikali ili wapate elimu bora.

Millanzi amesema, matarajio ya Halmashauri ya Manispaa ya Matwara Mikindani ni kuandikisha watoto 1922 kwa darasa la awali, na mpaka sasa wameshafikia lengo la uandikisha kwa asilimia 100 za uandikishaji na wanawaomba watoto hao waweze kuripoti shuleni kwa ajili ya kuanza masomo.

Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani iliweka maoteo/matarajio ya kuandikisha watoto wa darasa la awali 1,922 kwa mwaka wa masomo 2023, ambapo wameweza kuvuka lengo la idadi ya uandikishaji.

Matarajio ya uandikishaji kwa watoto wa darasa la kwanza kwa mwaka 2023, Manispaa ya Mtwara Mikindani ilitarajia kuandikisha watoto 2,556 na katika zoezi hilo wameweza kufanikisha nakuvuka lengo la uandikishaji.

Blandina Japhet mzazi na mkazi wa mtaa wa Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema, zoezi la uandikishaji kwa mwaka huu limekuwa tofauti na miaka ya nyuma na imepelekea baadhi ya wazazi na walezi kutokupata taarifa kwa wakati.

Tumezoea huwa tunawaandikisha watoto mwezi wa 12 mpaka januari wakati shule zimefunguliwa, ila kwa mwaka huu ytaratibu umebadilika na umetushitukiza na baadhi ya watoto walikuwa wapo kwenye jando na unyago vijijini, na msimu wa unyago na jando shughuli nyingi