Jamii FM

Balozi wa Sweden atembelea Waandishi wa Habari Mtwara

28 July 2022, 19:12 pm

Balozi wa Sweden ūüáłūüá™ nchini Tanzania Anders Sj√∂berg, leo julai 28,2022 ametembelea katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) zilizopo katika jengo la Chama cha waalimu – CWT, mkoani humo.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg, leo julai 28,2022 akiwa katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC)

Balozi wa Sweden akiwa na viongozi wa waandishi wa Habari Mkoani Mtwara

Balozi huyo amepokelewa na viongozi wa Chama hicho wakiongozwa na Katibu msaidizi Gregory Millanzi pamoja na Mratibu Abdallah Nassoro.

Ziara hiyo ya Balozi Anders ina lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Nchi ya Sweden na Chama cha waandishi wa habari mkoani Mtwara.

Katika mazungumzo yao, viongozi wa MTPC wamepata nafasi ya kueleza mafanikio na changamoto za Wanahabari wa Mkoa wa Mtwara.

Sweden ni wadau na wafadhili wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC, kupitia shirika la maendeleo la watu wa Sweden SIDA.