Jamii FM

Mtwara wahakikishiwa huduma bora za maji

11 January 2021, 16:22 pm

Waziri wa Maji Juma Aweso amefanya ziara ya kikazi ya siku Moja Mkoani Mtwara kukagua utekelezaji wa miradi ya maji na amewahakikishia wananchi wa Mtwara hatakuwa na kikwazo katika kuwaletea huduma bora za Maji safi na salama.

Waziri Aweso ameyasema hayo Januari 09 2021, alipokuwa Manispaa ya Mtwara Mikindani na wilaya ya Newala, pia katika ziara hiyo amewataka MTUWASA na RUWASA kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi ya Maji ili ikamilike kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

Miongoni mwa miradi aliyotembelea ni pamoja na mradi wa ujenzi wa chujio uliopo Mangamba ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mradi wa Makonde uliopo Wilaya ya Newala huku akisema serikali imejipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kupitia chanzo cha mto Ruvuma.