Jamii FM

Mashujaa waomba kazi zao zienziwe

26 July 2023, 07:41 am

Tunaiomba Serikali kutosahau Mashujaa tuliopo na kuenzi kazi tulizozifanya kwa taifa letu

Na Msafiri kipila

Kila Ifikapo Julai 25 ya Kila mwaka Tanzania huadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambapo kitaifa imeadhimishwa katika Uwanja wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma huku Mgeni Rasmi ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Picha ya pamoja viongozi na wanajeshi mkoani Mtwara. Picha na Msafiri kipila

Mkoani Mtwara Kumbukumbu hizo zimefanyika Katika Makaburi ya Mashujaa Na kuhudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbasi pamoja na Viongozi Mbalimbali ambapo zimefanyika julai 25, 2023

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kanali Ahmed Abbasi

Baadhi ya ndugu wa mashujaa waliofika katika kumbukumbu hizo wamesema wanaipongeza Serikali kwa kuenzi Mashujaa hao kila ifikapo 25 Julai.

Sauti ya ndugu wa mashujaa

Kwa niaba ya wastaafu Meja mstaafu Mohammed Bakari Mbwana ameiomba Serikali kutowasahau Mashujaa hao na kuenzi kazi walizozifanya kwa Taifa lao

Sauti ya Meja mstaafu Mohammed Bakari Mbwana
Picha ya viongozi mbalimbali kwenye siku ya mashujaa. Picha na Msafiri kipila