Jamii FM

Siku ya mwanamke anayeishi kijijini

17 October 2023, 14:25 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) Tanzania Komba Baltazar. Picha na Musa Mtepa

Suala la ukatili bado linaendelea  katika jamii huku suala la undugu likiwa kikwazo kutokomeza, wanajamii wamekuwa wakifichiana matukio hayo hasa  rushwa ya ngono katika maeneo ya kazi na taasisi za elimu.

Na Musa Mtepa

Wananchi  mkoani Mtwara wametakiwa kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kujitokeza katika jamii  kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka za kisheria na kuachana na tabia ya kumalizana kindugu.

Kaimu katibu tawala ambae pia ni katibu tawala mzaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Mtwara Bi. Nanjiva Mzunda akizungumza katika maadhimisho hayo. Picha na Musa Mtepa

Akimwakilisha mkuu wa mkoa kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke aishie kijijini yaliyofanyika Oktoba 15, 2023 katika kijiji cha Msangamkuu mkoani Mtwara, Kaimu Katibu Tawala mkoa ambaye pia ni katibu tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji  Bi. Nanjiva Geofrey Nzunda amesema kuwa ili kukomesha suala la ukatili wa kijinsia kwa yule aliyefanyiwa  ukatili kuwa tayari kuripoti na kutoa ushirikaano hasa pale linapofikia katika vyombo vya sheria.

Sauti ya Kaimu katibu tawala mkoa Bi Nanjiva Geofrey Nzunda

Aidha Bi Nzunda amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Dawati la Ustawi wa Jamii katika mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha January 2022 hadi June 2023 jumla ya matukio 1568 yameripotiwa  yakiwemo ya watu wazima 638, Wanawake 517 na wanaume 121  waliofanyiwa vitendo vya ukatili  huku ukatili wa kijinsia ukiongoza kwa kuripotiwa matukio 419.

Sauti ya Kaimu katibu tawala mkoa Bi Nanjiva Geofrey Nzunda

Kwa upande wake  Afisa Mipango na utawala kutoka shirika la Door Of Hope Tanzania  Jesca Muhagama amesema kupitia maadhimisho  hayo wamegundua kuwa suala la ukatili bado linaendelea  katika jamii huku suala la undugu likiwa kikwazo kutokomeza kwani Wanajamii wamekuwa wakifichiana matukio hayo hivyo wao kama shirika wamekuwa wakipambana na vitendo hivyo  hasa  Rushwa ya Ngono Makazini na taasisi za Elimu.

Sauti ya Afisa Mipango na utawala kutoka shirika la Door Of Hope Tanzania Bi Jesca Muhagama

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Faidika Wote Pamoja FAWOPA Tanzania Komba Baltazar amesema kupitia maadhimisho hayo wametoa Elimu kwa Wanawake kuhusiana na haki yao ya msingi ya kutafuta haki mahali popote pale kwenye mamlaka za haki na kuzitaka mamlaka zinazotoa haki kumzingatia Mwanamke wa  vijijini kumuhudumia mapema pale anapoenda kwenye mamlaka husika, hospitali au kwenye Dawati la jinsia kumpatia kipaumbele cha kumuhudumia mapema zaidi.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) Tanzania Komba Baltazar

Akielezea sababu zinazopelekea kutotoa taarifa hasa pale matukio ya kiukatili wa kijinsia yanapotokea katika jamii hususani vijijini Salima Mohamed Katulituli ambaye ni katibu wa kikundi cha Tukamulane Utamaduni na Mazingira amesema kuwa tatizo kubwa ni uwepo wa woga wa kutoa taarifa kwa kufikiri kuwa huenda akazungumzwa vibaya pale atakapobainika kuwa ndie alietoa taarifa hiyo.

Sauti ya katibu wa kikundi cha Tukamulane Utamaduni na Mazingira Bi. Salima Mohamed Katulituli

Haya ni maadhimisho ya Siku ya Mwanamke wa kijijini yaliyoanzishwa Mwaka 2018 yakiwa na lengo la kutambua mchango wa Mwanamke wa  kijijini katika kuboresha uchumi wa Tanzania na kwa mkoa Mtwara Mwaka huu yakifanyika katika kijiji cha Msangamkuu Halmashauri ya Wilaya na mkoa wa Mtwara.